Ni miaka mingi sana tulikuwa hatusikiki,
Hata ikawa vigumu kwa watu kutambua uwepo wetu,
Hivi leo nasi tu watu, tunapendeza na imepita enzi ya eti tulikuwa hatutamaniki,
Ni kwa mapambano tu yaloleta uwepo na utu wetu,
Tumedhamiria sasa kujitangaza na hii tutafanya hadi tutapofariki,
Tumejitoa muhanga kutetea na kuchangia kwa maslahi ya watu wetu,
Tumechoshwa na enzi zile za unafiki na hasa yale majabali ya uzandiki,
Tutaendelea na kazi tunayoianza na katu hatutawatupa mlio toa imani kwetu,
Hatutalala tukisikiza kilio na njaa zenu, vivyo hivyo tutawalinda katikati ya dhiki.
Tuliaminishwa kuweza na katu hatutathubutu kula nyama za watu,
Tutasema kweli daima bila kikomo na tutasimamia haki.